The House of Favourite Newspapers

VIONGOZI CHADEMA WAWASILI SENTRO

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Vincent Mashinji na viongozi wenzake ameripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi (Centro) kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa kwenye kesi yao uchochezi inayowakabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 

Akizungumza na waandishi mara baada ya kutoka ndani ya kituo hicho, Mashinji amesema kuwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya pindi wanaporipoti kituoni hapo, ni kuitikia wito na kusaini kwenye kitabu kilichopo kwenye kituo hicho na baadaye kuondoka kila Ijumaa. Wabunge wengine waliowasili ni Peter Msigwa, John Heche na Ester Matiko.

 

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe.

Comments are closed.