Viongozi mbalimbali Wahudhuria hafla ya ya kumuaga Rais wa Poland Ikulu Dar – Picha
Rais Samia Suluhu Hassan amesema timu ya wataalam imeshaelekezwa kuchukua hatua zitakazowezesha kuanza kwa safari za moja kwa moja kati ya Poland na Tanzania.
Aidha, Rais Samia amesema safari hizo zitachochea zaidi utalii pamoja na biashara kwa kuwa Poland ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kuwa na watalii wengi nchini.
Rais Samia amesema hayo leo Ikulu akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Poland, Andrzej Duda aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku 2 wakati wakizungumza na vyombo vya habari.
Vile vile, Rais Samia amewakaribisha wawekezaji kutoka Poland kuchangamkia fursa za uwekezaji kwenye sekta ya utalii hususan ujenzi wa hoteli.
Rais Samia pia amesema Tanzania na Poland zitaendelea kushirikiana katika sekta za elimu na kuhamasisha uwekezaji zaidi kwenye sekta za kimkakati kama vile viwanda, uzalishaji, nishati, madini, gesi asilia na uchumi wa buluu.