The House of Favourite Newspapers
gunners X

Virusi vya Corona Vyatua Ufaransa, Afrika Yaanza Kudhibiti

0

SERIKALI ya Ufaransa imetangaza visa vya maambukizi ya virusi vya corona vilivyoanzia nchini China ambapo watu watatu wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo vinavyosababisha homa na vilivyoathiri mamia nchini China.

 

Kulingana na taarifa za jana za wizara ya afya ya Ufaransa, wawili ni kutoka mji mkuu wa Paris na mmoja ni kutoka mji wa Bordeaux. Mamlaka za afya zinajaribu kubaini watu wengine waliokuwa na maingiliano na wagonjwa hao watatu waliambuklizwa virusi vya corona.

 

Wizara ya afya imewasisitiza wale wanaowajua wagonjwa hao kujichunguza wenyewe iwapo wana dalili zozote za maambukizi na kuwataka wabakie majumbani mwao wakiamini nao wameambukizwa.  Hayo yakijiri, nchini Marekani mgonjwa wa pili amethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo vya corona jana Ijumaa.

 

Aidha, Mataifa kadhaa ya Afrika yameanzisha upimaji wa joto la mwili katika viwanja vya ndege na kuchukua hatua za tahadhari kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema inachukua hatua za tahadhari katika viwanja vya ndege na bandari zikiwalenga watu wanaotoka mataifa yaliyoathirika na virusi hivyo.

 

Nigeria, Uganda, Ghana na Ushelisheli pia zimetangaza mipango ya kuchukua hatua kama hizo kukabiliana na virusi vya Corona ambapo wasafiri watapimwa joto la mwili kubaini dalili za maambukizi ya virusi.

 

Taasisi ya magonjwa ya mripuko nchini Afrika Kusini imesema bado haijaweka mifumo ya kupima watu kwenye maeneo ya kuingia nchini humo lakini imewataka raia wote waliokuwa China hivi karibuni kufanya uchuguzi wa Afya.

 

Leave A Reply