The House of Favourite Newspapers

VISIWA VINACHOKABILIANA NA MAGONJWA HATARI DUNIANI

Kisiwa ndani ya sehemu ya Bijagos

Wasafiri wanaozuru visiwa vya barani Afrika vinavyofahamika kama Bijagos wanatarajia kujionea mandhari ya kipekee ya fukwe za kale na misitu asilia. Lakini uzuri wa visiwa hivyo hauishii hapo, kwani pia vinatumika kama maabara asilia kutokana na mazingira ya kipekee ambayo yanafanyiwa utafiti wa baadhi ya magonjwa hatari ya duniani. Mkusanyiko wa visiwa 18 kutoka pwani ya Bijagos nchini Guinea-Bissau, barani Afrika Magharibi, ni makazi ya watu 30,000 wanaotumia lugha zao na mila za pekee. Pia wanaishi karibu na wanyama pori na viboko wa kipekee wanaoishi katika wa maji ya bahari na kasa wakubwa.Islander Ansulmani akichukua vilui lui vya mbu katika kidimbwi cha maji

Lakini visiwa hivi vya kupendeza vinakabiliwa na magonjwa ya kila aina ambayo yanatishia maisha ya wenyeji. Muda wa kuishi wa watu nchini Guinea-Bissau ni miaka 60, lakini katika visiwa vya Bijagos inaaminiwa kuwa chini kidogo. Magonjwa yanayo wahangaisha watu ni pamoja na malaria, ugonjwa wa macho unaofahamika kama trachoma, matende na minyool  Hata hivyo visiwa hivyo huenda vina siri ya kukabiliana na magonjwa hayo ipasavyo.

Watafiti wa matibabu wamekuwa wakifanya kazi katika visiwa vya Bijagos kwa miaka kadhaa kubaini ikiwa wanaweza kuangamiza baadhi ya magonjwa katika visiwa hivyo. Hii ni kwa sababu visiwa hivyo vinahudumu kama maabara asilia kutokana na uhalisia wake. Japo hali hiyo inafanya maisha ya kila siku ngumu, inasaidia katika juhudi za kuangamiza magonjwa.Kiboko anayeishi ndani ya maji ya chumvi Bijagos

Maji yanayotenganisha visiwa hivyo yanatumika kama kinga asili. Hali hiyo inasaidia kulinganisha mbinu tofauti za kudhibiti magonjwa bila hatari ya kuharibu majaribio katika maeneo mengine ya utafiti. Katika maeneo mbalimbali watu wanaweza kuingia na kutoka sehemu zinazofanyiwa majaribio ya tiba hali ambayo inafanya kuwa ngumu kubaini chanzo na athari ya magonjwa hayo. Japo kuna visiwa vingi duniani ni vichache vinakaribiana. Hii inasaidia watafiti kufanya kazi tofauti lakini vikiwa mbalimbali ni bora zaidi kwa sababu uwezekano wa majaribio ya utafiti kuharibiwa ni mdogo sana.Boti kutoka bandari ya Bissau ikijiandaa kwa safari ya Bijagos

Watafiti kutoka chuo cha London kinachoshughulikia masuala ya usafi na tibi ya dawa za tropiki (LSHTM) awali ilikuwa inaangazia ugonjwa wa macho unaofahamika kama trachoma. Ugonjwa huo unawakabili watu milioni 1.9 duniani na ni moja ya hali ambayo inasababisha upofu unaoweza kutibiwa. Trachoma unaweza kuambukizwa kupitia mikono iliyogusa macho ya mgonjwa, nguo zake au kupitia inzi aliyekalia jicho la mgonjwa.Dkt Anna akimhudumia mgonjwa aliye na matatizo ya macho

Hali hiyo huwaathiri zaidi watu wanaoishi katika mazinga machafu. Ugonjwa huo umeathiri mataifa 42 duniani. Kuna wakati mmoja kulishuhudiwa visa ambapo kila mtoto katika vijiji vya kisiwani walikabiliwa na ugonjwa huo.   Dkt Anna Last kutoka taasisi ya LSHTM aligundua maeneo yaliyokuwa katika hatari ya ugonjwa wa trachoma kabla ya kutibu jamii nzima kwa kutumia anti-bayotiki ili kukomesha mzunguko wa maambukizi.Watafiti wa LSHTM wakiondoka kisiwa cha Rubane baada ya kufanya utafiti wa mbu

Ugonjwa wa trachoma, ambao ni chanzo cha hali inayosababisha kupofuka macho si tatizo pekee linalowakabili watu.    Katika visiwa vya Bijagos, kuna magojwa mengine kadhaa ambayo yanashughulikiwa. Kwa sasa panaangaziwa ugonjwa wa malaria ambao unasambazwa na mbu. Dawa mpya ya kukabiliana na mbu inatarajiwa kufanyiwa majaribio. Tiba zilizopita zilikuwa zinalenga kukabiliana na vimelea vya malaria ndani ya mwili wa binadamu.

Comments are closed.