Vita: Simba Leteni Bil 2 Tuwape Makusu

JeanMarc Makusu

KOCHA Mkuu wa AS Vita Club, Florent Ibenge amesema kama Simba inataka kumsaini JeanMarc Makusu basi wala hakuna shida watoe dola 1,000,000 (Sh bil 2.3).

 

Simba imeripotiwa kumfukuzia Makusu ambaye amekuwa kwenye kiwango bora katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo inataka kumsaini kwa ajili ya msimu ujao.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ibenge ameweka wazi kwamba, Makusu amekuwa akitakiwa na moja ya timu za Comoro lakini kama Simba wakimtaka hakuna shida ikiwa watafi kia thamani hiyo.

Aidha aliongeza kama Makusu atakwenda Comoro basi wao chaguo lao la kwanza ni Meddie Kagere wa Simba au Clatous Chama na Emmanuel Okwi.

 

“Makusu kuna timu kutoka Comoro inamhitaji lakini pia Simba inaweza kumpata kama itatoa dola mil moja,” alisema Ibenge na kuongeza kuwa: “Katika mchezo wetu na Simba ni wa kawaida sana, siogopi chochote na kama wakikaa vibaya tunaweza kupata ushindi wa mabao 5-0 kama ule wa kwanza. Nimesikia wanasema Zahera anatusaidia, hiyo kitu haina ukweli wowote.”

Wilbert Molandi na Ibrahim Mussa | Championi

Toa comment