The House of Favourite Newspapers

Vita vya Ukraine: Joe Biden Afutilia mbali Uwezekano wa Kuipa Ukraine Ndege za Kivita za F-16

0

Rais wa Marekani Joe Biden amefutilia mbali uwezekano wa kutuma ndege za kivita za F-16 nchini Ukraine, licha ya wito mpya kutoka kwa maafisa wa Ukraine wa kuomba msaada wa ulinzi wa anga.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari Jumatatu ikiwa Marekani itatoa ndege hizo, Bw Biden alijibu kwa urahisi “hapana”.

Kauli yake inakuja siku moja baada ya kiongozi wa Ujerumani pia kukataa kutuma ndege za kivita.

Ukraine imesema inahitaji ndege hizo kuchukua udhibiti wa anga yake katika vita vinavyoendelea dhidi ya Urusi.

F-16 Fighting Falcons inachukuliwa sana kuwa mojawapo ya ndege za kivita zinazotegemewa zaidi duniani na hutumiwa na nchi nyingine, kama vile Ubelgiji na Pakistan.

Zitakuwa uboreshaji mkubwa kwenye ndege za kivita za enzi ya Usovieti zinazotumiwa na Ukraine hivi sasa, ambazo zilitengenezwa kabla ya nchi hiyo kujitangazia uhuru kutoka kwa USSR zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Hata hivyo, Bw Biden amepinga mara kwa mara ombi la Ukraine la kutaka ndege hizo, badala yake akalenga kutoa msaada wa kijeshi katika maeneo mengine.

Marekani ilitangaza wiki iliyopita kuwa itaipatia Kyiv vifaru 31 vya Abrams, huku Uingereza na Ujerumani pia zikiahidi msaada sawia na huo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Melnyk, alikaribisha tangazo hilo lakini akaomba washirika kuunda “muungano wa ndege za kivita” ambao pia utaipatia Ukraine ndege za Eurofighters, Tornados, Rafales za Ufaransa na ndege za Gripen za Uswidi.

Katika mahojiano siku ya Jumapili , Kansela wa Ujerumani alisema “ilionekana kuwa ni ujinga” kujadili kutuma msaada mwingine wa kijeshi kwa Ukraine wakati walikuwa wamejitolea kutuma vifaru vya Leopard 2.

Olaf Scholz pia alikariri gazeti la Ujerumani la Tagesspiegel kwamba muungano wa kijeshi wa Nato haukuwa na vita na Urusi na kwamba “hautaruhusu kuongezeka kwa mzozo huo kwa njia kama hiyo”.

BREAKING: YANGA YATAMBULISHA JEZI MPYA KUELEKEA MICHUANO ya CAF, ZINAUZWA ELFU 50…

Leave A Reply