testiingg
The House of Favourite Newspapers

Vita vya Ukraine: Poland Yaiomba Ujerumani Ruhusa Kusafirisha vifaru hadi Ukraine

0

Poland imeiomba rasmi Ujerumani ruhusa ya kusafirisha vifaru vingi vya vita aina ya Leopard 2 kwenda Ukraine hatua ambayo inaibua shinikizo kwa Berlin kufanya uamuzi kuhusu suala hilo gumu.

Serikali ya Ujerumani imepokea ombi la kusafirisha vifaru 14 viliyotengenezwa Ujerumani siku ya Jumanne.

Lakini imesisitiza uamuzi wa mwisho ni wa Kansela Olaf Scholz.

Ukraine inaona mizinga hiyo kuwa muhimu kwa kuvunja mistari ya Urusi na kushinda shambulio lolote linalopangwa.

Vifaru vya Leopard 2 viliundwa mahsusi kushindana na vifaru vya urusi aina ya T-90, ambavyo vinatumika katika uvamizi. Lakini sheria za usafirishaji zinamaanisha nchi yoyote ambayo inataka kutuma mizinga hiyo inahitaji kibali cha Berlin.

Waziri mkuu wa Poland Masteusz Morawiecki alisema anatumai Ujerumani itajibu ombi hilo haraka, na kuishutumu Ujerumani kwa “kuchelewesha, kukwepa, kutenda kwa njia ambayo ni ngumu kuelewa”.

Pia alisema Poland itaomba Umoja wa Ulaya kufidia gharama ya mizinga inayotaka kupeleka Ukraine.

Ujerumani imekuwa ikisita kutuma magari hayo, au kuruhusu mataifa mengine kufanya hivyo, huku moja ya wasiwasi wake ikiwa ni hofu kwamba hatua ya ghafla kuhusu suala hilo inaweza kuzidisha mzozo kati ya Urusi.

Siku ya Jumanne Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorious alisema Berlin imewapa mataifa washirika ruhusa kuwafunza raia wa Ukraine kutumia vifaru vya Leopard 2, lakini hawakujitolea kutuma vyao.

BIMA ya AFYA kwa WOTE, WAZIRI UMMY MWALIMU AFUNGUKA WATANZANIA WATAKAVYONUFAIKA…

Leave A Reply