The House of Favourite Newspapers

Vita ya Mastaa Bongo, Simba vs Yanga

0

KIMEUMANA! Ndivyo unavyoweza kusema kuelekea Dabi ya Kariakoo kati ya timu pendwa Bongo za Simba na Yanga hiyo leo katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo vita ya mastaa mashabiki wa timu hizo, imeibuka upya.

 

Mchezo huo umeibua tena vita ya kiburudani kwa mara nyingine kwa baadhi ya mastaa wa kiume na kike Bongo ambao wanajihusisha na fani nyingine kama muziki na filamu ambao ni mashabiki wa timu hizo.

 

Baadhi ya mastaa wapo Simba na wengine ni Yanga hivyo tambo, majivuno, vijembe na mengineyo lazima viibuke kama ilivyo jadi zinapokutana timu hizo na hicho ndicho kinachoendelea.

 

Wale wa Klabu ya Simba wakiongozwa na Mwijaku wameendelea kutambiana na wale wa Yanga wanaaongozwa na Baba Levo.

 

Wawili hao wanaofanya sanaa na utangazaji wa redio, wamekuwa katika vita vya maneno ambapo Baba Levo anapambana na yeyote anayemshambulia Diamond Platnumz huku Mwijaku akifanya hivyo kwa yeyote anayemgusa Harmonize.

 

Hata hivyo, hapa pamekuwa na songombingo kwa sababu, Baba Levo yupo upande wa Diamond ambaye ni shabiki kindakindaki wa Mnyama huku Mwijaku naye akiwa upande wa Harmonize ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Wananchi. Patamu hapo!

 

Mastaa wengine wa kiume waliopo upande wa Simba wanaopambana katika vita ya maneno na wale wa Yanga ni pamoja na Marioo, Billnass, Joh Makini, Whozu, Meja Kunta, Ben Kinyaiya, Mwasiti, JB, Quick Rocka na wengine.

 

Kwa upande wake, mwanamitindo Hamisa Mobeto na mwigizaji Monalisa wamekuwa wakitajwa kuongoza tambo za mashabiki wa Simba kwa upande wa mastaa wa kike.

 

Mobeto na Monalisa wanakabiliana na tambo za akina Wema Sepetu, Shilole, Nandy, Kajala Masanja, Riyama Ally, Irene Uwoya, Malaika, Zamaradi, Jacqueline Wolper na wengine ambao ni mashabiki wa Yanga.

 

Mchezo huo wa kukata na shoka ambao upande mmoja lazima ulale na maumivu, utapigwa kwenye Dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar, leo, kuanzia muda wa saa 11:00 jioni kuashirikia kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply