VITA YA PENZI HAIJAWAACHA SALAMA

MAISHA ni safari ndefu. Kuna kupanda na kushuka. Kuna furaha na huzuni.  Kwenye ulimwengu wa mastaa hapakosekani vitimbi na mikasa ya hapa na pale.

 

Kwa watu wa kawaida huwa yanatokea mambo mengi vivyo hivyo kwa mastaa pia ila wanaonekana zaidi kwa kuwa wao ni kioo cha jamii na watu wengi wanawafuatilia maisha yao.

 

Katika makala haya leo tunakuletea mastaa wa Bongo ambao wameingia kwenye vita ya penzi baada ya kuchukuliana wapenzi wao. Unajua hata kama umeachana na mtu kama ulikuwa bado unampenda au labda mmewahi kupata watoto, ukiona mtu anamchukua na kuwa naye kimapenzi lazima kuna maumivu fulani mtu huyapata.

 

 

Hii imewakuta mastaa hawa hapa chini na kujikuta wakiingia kwenye ugomvi na kuwa na bifu kubwa huku wengine wakigeuka kuwa maadui wakubwa wakati awali kabla ya kuchukuliana wapenzi walikuwa marafiki wazuri.

 

WEMA NA KAJALA

Wasanii wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja waliingia kwenye bifu baada ya Wema kudai kwamba Kajala amemchukulia aliyekuwa mpenzi wake kipindi hicho aliyejulikana kwa jina la CK.

 

Kabla hayajatokea hayo, Wema na Kajala walikuwa marafiki wa kupika na kupakua kwani walikuwa wakiambatana kila sehemu kama kumbikumbi, hii ni baada ya Wema kumwokoa Kajala na kifungo mahakamani ambako alimtolea shilingi milioni 13 za faini na kuachiwa huru.

 

Baada ya Kajala kumchukua mpenzi wa Wema hadi leo wawili hawa ni kama paka na panya kwani hawaelewani hata kidogo. Wema amekuwa akipata majanga mbalimbali, lakini Kajala haonekani hata kumpa pole wala kumjali.

NISHA NA SNURA

Mwanamama Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye ni msanii wa filamu Bongo na mwanamuziki, Snura Mushi nao ni mahasimu walioingia kwenye gogoro zito la penzi. Wasanii hawa hadi sasa hawapendani ikiwa ni baada ya Snura kudaiwa kumchukua aliyekuwa mpenzi wa Nisha aliyejulikana kwa jina la Minu japokuwa kwa sasa walishaachana.

 

Awali Snura alijitetea kwamba mwanaume huyo ni mtu wake wa karibu tu na siyo mpenzi wake, lakini baadaye waliweka mapenzi yao wazi na kusema kuwa mwanaume huyo alikuwa ameshaachana na Nisha ndiyo maana akawa naye.

DIAMOND NA DIMPOZ

Hawa ni mastaa wa Bongo Fleva ambao vita yao inazidi kuwa kubwa kila kukicha kwani wana bifu la muda mrefu sasa.

 

Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliingia kwenye vita ya penzi na Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ baada ya Dimpozi kudai kuwa ametoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu ikiwa ni baada ya picha zao wakiwa kimahaba kitandani kuvuja mitandaoni. Kwa wakati huo Diamond na Wema walikuwa wametengana, lakini ilionekana bado alikuwa akimpenda hivyo kuzua vita.

 

Pamoja na hilo pia bifu liliongezeka baada ya Dimpoz kumtaka Diamond amwite baba kwa kile kilichodaiwa kuwa amewahi kutoka na mama yake hivyo Diamond akakasirika zaidi na urafiki wao ukaishia hapo. Kama hiyo haitoshi bado wawili hao wanachokozana ikiwa ni baada ya Dimpoz kuonekana akiwa karibu na mama watoto wa Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni raia wa Uganda.

 

Dimpoz amekuwa akionekana mara kwa mara akiwa amepiga picha na Zari na hivi karibuni walionekana wakiwa kwenye picha ya pamoja nchini Kenya huku wakijirekodi video mbalimbali wakiwa wanaimba ambazo zilisambaa mitandaoni.

MOBETO NA TAHIYA

Mwanamitindo Hamisa Mobeto na mwenzake, Tahiya waliingia kwenye vita nzito ya maneno baada ya kuchukuliana bwana.

 

Tahiya alidai kuibiwa bwana na Mobeto ambapo alimchimba mkwara kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa aachane na mwanaume wake, lakini baadaye vita ikawa kubwa baada ya mwanadada huyo kudai kumfumania Mobeto hotelini akiwa na mwanaume wake.

CHUCHU HANS NA JOHARI

Chuchu Hans na msanii mwenzake wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ ni mahasimu kwani hawapendani chanzo kikidaiwa ni penzi.

 

Licha ya kwamba hawajawahi kuanika hadharani Johari na Vincent Kigosi ‘Ray’ ambao wanaunda Kampuni ya RJ inayojishughulisha na filamu walikuwa wapenzi kwa muda mrefu.

 

Penzi lao linadaiwa lilivunjika baada ya Chuchu Hans kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray ambapo walijaliwa mtoto mmoja licha ya hivi karibuni habari kueleza kuwa wameachana. Johari na Chuchu hadi sasa hawapendani na hawachangamani kabisa, kisa kikidaiwa ni hilo penzi la Ray.

MAKALA: GLADNESS MALLYA

DUNIA IMEKWISHA! Mtoto AMBAKA Mama Yake MZAZI, Polisi WAMNASA!


Loading...

Toa comment