The House of Favourite Newspapers

Viwanda vya Nyerere Vyamtesa JPM, Alia na Mafuta Machafu Nchini – Video

 

RAIS wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza masikitiko yake kutokana na viwanda vingi vilivyoachwa na Rais wa kwanza, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada vikabinafsishwa, kutelekezwa na kufa.

 

Hayo ameyaeleza leo Machi 15, 2018 katika uzinduzi wa kiwanda cha sigara cha Philip Moris mjini Morogoro, na kuwataka Watanzania kubadilika kwa kuwekeza katika viwanda.

 

“Viwanda vyote vilivyoachwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama vingekuwepo, leo tusingekuwa na tatizo la ajira, sababu wasomi tunao wa kutosha, vijana tunao wa kutosha. Unapokuwa na kiwanda halafu kikafungwa unakuwa umepoteza ajira za Watanzania waliokuwa wakifanya kazi hapo

 

“Tunapokuwa na kiwanda kama hiki chenye uwezo wa kuzalisha sigara milioni mia nne kwa mwaka nina uhakika wakulima wetu wote wanaolima tumbaku watakuwa na soko nzuri. Nimeshatoa maelekezo kwa Waziri wa Viwanda  na wa Fedha waangalie kodi ambazo zinaleta kero kwa  viwanda vyetu,” alisema Rais Magufuli.

 

Aidha, akizungumzia suala la mafuta yanayoingizwa nchini, Rais amesema:

“Watu wamekuwa wakiagiza ‘crude oil’, wanadai ni ‘crude oil’ wakati ni mafuta ambayo ni semi-refined. Wanakuja wanayauza hapa kwa bei ya chini na viwanda sasa vinashindwa kushindana na bei ya mafuta kutoka nje.

 

“Mafuta kutoka nje yanakuwa na ubora wa ajabu, mengine yanakuwa tayari yame-expire. , ndiyo maana Watanzania tunakula mafuta ya ajabuajabu baadaye tunapata magonjwa ya ajabuajabu, mara kansa, mara nasikia tutumie dawa za vijana.”

 

Na Edwin Lindege.

VIDEO: HOTUBA YA RAIS MAGUFULI WAKATI

Comments are closed.