Vodacom kuwarejesha Vifurushi Wateja Waliokosa Huduma ya Intaneti Tangu ilipokatika
Kampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania imesema imefanikiwa kurejesha Mawasiliano yote ikiwemo Huduma ya Intaneti iliyokatika kwa siku kadhaa, na itaanza kuwarejeshea Vifurushi Wateja wote waliolipia na kukosa Intaneti
Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa VodacomTanzania imeeleza Kampuni inatambua usumbufu uliojitokeza na inawaomba radhi Wateja wake kutokana na tatizo hilo