The House of Favourite Newspapers

Vodacom Tanzania ilivyoadhimisha Siku ya Wanawake Duniani

0

vodacom Tanzania (1)

Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Evans Lyimo (kushoto) akimuuliza swali Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Chris Mauki (hayupo pichani) wakati alipokuwa akiongea na wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo kuhusiana na jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

vodacom Tanzania (2)

Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Chris Mauki (kulia) akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa Vodacom Tanzania ya jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

vodacom Tanzania (3)

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakionesha mshikamano katika Siku ya Wanawake Duniani yenye lengo la kuwawezesha. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Bi. Zuhura Muro ambaye alitoa uzoefu wake na kuweka mkazo zaidi kwenye suala la kumudu kazi wanazozifanya ikiwemo suala la kujiamini ambapo alisema ni mambo ya muhimu katika msukumo wa kuleta usawa wa kijinsia.

vodacom Tanzania (4)

Afisa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Perece Kirigiti akiongea na wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuhusu mada kuu ya mwaka 2016 ya Siku ya Wanawake Duniani “ Fursa na Usawa kwa wote” katika hafla ya kifungua kinywa iliyofanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania.

Vodacom Tanzania ilianza maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani kwa kuwa na mafunzo yanayohusiana na masuala ya jinsia yenye mwelekeo wa kuleta usawa wa kijinsia sehemu za kazi kwa wafanyakazi wa kampuni.

Mafunzo ya wanawake yalihusu jinsi wanavyoweza kushirikiana kuinuana kiuchumi. Bi.Zuhura Muro, kutokana na uzoefu wake mkubwa alipata fursa ya kuwaelimisha na kuwashauri wafanyakazi masuala mbalimbali yanayoweza kuwaletea mafanikio ambapo aliweka mkazo zaidi kwenye suala la kumudu kazi wanazozifanya ikiwemo suala la kujiamini ambapo alisema ni mambo ya muhimu katika msukumo wa kuleta usawa wa kijinsia.

Mafunzo ya wafanyakazi wanaume yalijikita zaidi ni jinsi gani wanaume wanaweza kuwawezesha wanawake na yalitolewa na Mtaalamu wa Saikolojia na Mahusiano Dkt.Chris Mauki,mtaalamu huyo aliwafundisha wafanyakazi wa kiume jinsi gani wanaweza kuwekeza kwa watoto wao wa kike zaidi ya kugharamia mahitaji yao kifedha ambapo aliwafundisha umuhimu wa kuwa karibu na watoto wao wa kike.Mafunzo hayo yaliyotoa fursa kwa wafanyakazi wa kiume kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na jinsia na mahusiano yaliwagusa wengi.

 

Leave A Reply