Vodacom Tusua Mapene Yamkabidhi Milioni Kumi Mkazi wa Tegeta jijini Dar

MKUU wa kitengo cha huduma za kidigitali Vodacom Tanzania, Goodluck Moshi akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa promosheni ya Vodacom Tusua mapene, Lilian Haule mkazi wa Tegeta jijini Dar es salaam, hafla ya makabidhiano imefanyika viwanja vya Zakhem Mbagala. Ili ushinde promosheni hii mteja wa Vodacom anatakiwa kutuma herufi V kwenda namba 15544 kuanzia gharama ya shilingi mia tatu na kuendelea. 

 

 

Mkuu wa kitengo cha huduma za kidigitali Vodacom Tanzania, Goodluck Moshi akizungumza na wakazi wa Mbagala waliojitokeza kushuhudia makabidhiano ya zawadi kwa mshindi wa promosheni ya Vodacom Tusua mapene, Lilian Haule ambaye amejishindia shilingi milioni kumi kutoka Vodacom.

 

 

Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Vodacom Tusua Mapene, Lilian Haule akizungumza na wakazi wa Mbagala waliojitokeza kushuhudia namna alivyokabidhiwa zawadi yake ya shilingi milioni kumi kutoka Vodacom.


Toa comment