The House of Favourite Newspapers

Vodacom Wadaiwa Kuvunja Mkataba Ligi Kuu

0

TETESI zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa msimu ujao haitaitwa tena Vodacom Primier Ligue (VPL) baada ya Vodacom kudaiwa kuvunja mkataba wa kuendelea kuwa mdhamini wa Ligi Kuu kwa sababu mbalimbali zilizoelezwa na uongozi.

 

Habari zinaeleza kuwa mabosi wa Vodacom wameona kwamba kuendelea na udhamini wa Ligi Kuu ya mpira wa Miguu Tanzania Bara kwao ni hasara.

 

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kampuni hiyo ambayo imekuwa ikidhamini Ligi Kuu kwa miaka 10 ilipata hasara kutokana na wateja wake zaidi ya milioni 2.9 kufungiwa laini zao kwa kushindwa kukamilisha usajili wa alama za vidole pamoja na sababu nyingine za kikodi.

 

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa wameamua kujitoa kutokana na kuona kwamba hasara kwao ni kubwa kuliko faida.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema kuwa hawezi kuongea juu ya suala hilo ikiwa litakuwepo watatoa taarifa.

Leave A Reply