VODACOM WASAIDIA WAJASIRIAMALI CHIPUKIZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi akizungumza na waandishi wa habari

Kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Vodacom ikishirikiana na Smart Lab wameamua kurudisha kwa jamii kwa kuwasaidia wajasiriamali chipukizi nchini. Kampuni ya Vodacom, leo imezindua program yake ya Vodacom Digital Accelerator yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na kuzalisha kipato.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar, leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa prorma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi amesema ushirikiano kati ya Vodacom na Smart Codes ni hatua katika kutoa fursa kwa wajasiriamali wanaoanza kwa kupitia sekta ya teknolojia.

Mkurugenzi huyo amewahamasisha vijana wengi zaidi kuwa wabunifu na kutumia fursa hii kama njia ya kujiwezesha kiuchumi kupitia katika kutatua matatizo ya maendeleo ya jamii katika jamii zao.

“Kampuni ya Vodacom mara zote inakusudia kuleta mabadiliko endelevu yenye manufaa kwa jamii ambako tunaendesha shughuli zetu sambamba na mtazamo wa mkakati wetu wa kibiashara na programu ya Vodacom Accelerator inakusudia kuthibitisha suala hilo,” alisema Hisham.

Na Neema Adrian
Toa comment