visa

Vodacom Washusha Gharama za Bando ‘Wajanja Hatuzimi Data’ – Video

Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa.

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania leo Alhamisi, Februari  13, 2020, wamezindua vifurushi vipya ya ‘Wajanja hawazimi Data’ ambapo mteja wao ataweza kujimwaga na Data kwa 25OMb kwa Tsh 500/= kwa saa 24, 3GB kwa Tsh 2,500/= kwa siku 3GB na 20GB kwa Tsh 15, 000/= kwa siku 7.

 

Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania, Linda Riwa, amesema kampeni yao hii mpya imelenga kuwanufaisha watanzania wa kipato cha chini ukilinganisha na vifurushi vya mitandao mingine  ambapo mteja anapata mara tatu ya Mb zinazopatika huko.

 

Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare,  amesema wameamua kuzindua menu  mpya ambayo ni kioo au mlango na kiunganishi kwa wateja wao kupata huduma baada ya kupokea malalamiko  kutoka kwa wateja wao.

Pia wameboresha vifurushi vya sauti ambavyo vitamwezesha mteja wa Vodacom kujimwaga kuongea ndani ya nchi na nje ya nchi.

Ili uweze kupata huduma hii utatakiwa kupiga *149*01# unachagua huduma ya nunua bando utachagua Internet utaona jimwage na Data.

 
Toa comment