Vodacom Yaendesha Droo ya Kwanza ya Sambaza Shangwe, Gusa Maisha
Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, leo imeendesha droo yake ya kwanza ya Kampeni ya Sambaza Shangwe, Gusa Maisha ambapo washindi 26 wamepatikana na kujishindia zawadi mbalimbali, ikiwemo mmoja aliyenyakua donge nono la shilingi milioni 10 taslimu.
Zawadi zinazoshindaniwa katika kampeni hiyo ni pamoja na bodaboda, runinga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na fedha taslimu.