The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yahitimisha Kampeni Ya Amsha Ndoto Kwa Kugawa Zawadi Kwa Wateja Wake

0
Meneja wa Huduma za Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Birgita Shirima akizungumza kwenye hafla hiyo.

Dar es Salaam 21 Januari 2023: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi inayoongoza hapa nchini Vodacom imehitimisha kampeni yake ya Amsha Ndoto kwa kuwazawadia wateja wake zawadi mbalimbali ikiwemo Smart Tv, Simu Janja, Router na Mamilioni ya Pesa kwa kufanya miamala ya M-Pesa.

Hafla ya kuhitimisha kampeni hiyo imefanyika Kituo cha daladala cha Mbagala Rangitatu jijini Dar na kuhudhuriwa na umati mkubwa uliofika kushuhudia tukio hilo.

Haji Abdallah (katikati) akionesha ishara ya ushindi wakati wakati akikabidhiwa Smart Tv na maofisa wa Vodacom.

Baada ya washindi kukabidhiwa zawadi zao Meneja wa Huduma za Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Birgita Shirima alisema;

“Leo hii Vodaco tumehitimisha kampeni yetu ya Amsha Ndoto, Amsha Shangwe kampeni hii tuliianza msimu wa sikukuu mpaka Januari hii ambapo tumeshatoa zawadi nyingi sana ikiwemo mshindi aliyekuwa akijiondokea na shilingi milioni kumi kila wiki kwa ajili ya kutimiza ndoto yake.

Fundi ujenzi Yusuph Abdallah mshindi wa shilingi milioni ishirini akizungumza kwa furaha baada ya kukabidhiwa pesa yake kwa njia ya MPesa.

“Lakini zaidi ya hapo, tulikuwa tunatoa zawadi ya shilingi milioni moja moja kwa washindi watano kila wiki na tumetoa Smart Tv ya kisasa kabisa kama mlivyoona na tulienda mbele zaidi kwa kuwapa wateja wetu ofa ya kusafiri na paisha bure na tulitoa ofa ya Voda Bima.

“Kwahiyo tulikuwa na mambo mengi sana mazuri kwa wateja wetu tangu kipindi cha sikukuu mpaka Januari hii.

“Tunaendelea kuwasisitiza wateja wetu wote waendelee kutumia huduma zetu za Mpesa kwani hizi huduma zinarahisisha kufanya miamala na kukufranya uwe salama kwa kukufanya usitembee na pesa taslimu.

Meneja wa Huduma za Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Birgita Shirima (kulia) na Masta Shangwe (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi.

“Huduma hizi tumezihimarisha na kukufanya uweze kupata huduma yoyote ya kifedha mahali popote, leo ukiwa na pesa kwenye MPesa huna haja ya kutafufa vocha unaweza kununua bando, muda wa maongezi, kufanya malipo ya serikali kama vile kulipia kodi, leseni, faini ambapo huduma hii inaisaidia serikali kupata mapato na serikali kukuza uchumi wetu.

“Sisi kama Vodacom Tanzania tunahakikisha tunatoa huduma zilizo bora ambazo zinakidhi mahitaji ya Watanzania ili tukuze uchumi maana tunaamini mawasiliano ni uchumi ndiyo maana pamoja na hayo mara kwa mara tumekuja vitu fulani vya kutimiza ndoto za wateja wetu.

“Ila kama unavyojua ukiwa namba moja ni lazima uwe zaidi kwa ubunifu na ndiyo maana mmeona tumekuja na mtandao wa kasi zaidi wa 5G ambao sisi ni wakwanza hapa Tanzania.

“Kwa hapa Dar es Salaam ukienda sehemu mbalimbali tumeshaweka hiyo minara na tumejikita pia na mikoa mingine kama vile Dodoma, Morogoro, Arusha, Tabora na sehemu nyingine pote huko tumeshaongeza hiyo kasi ya 5G, wewe ni nani usitumie mtandao huu wenye huduma zote bora hizo ambazo zimekurahisishaia maisha?

“Zaidi ya hapo leo kuna mtu kaondoka na shilingi milioni ishirini ya ‘Tusua Mapene’ na mwingine milioni kumi unaweza kupata wapi mtandao wa kukupa zawadi hiyo kipindi cha Januari hii?

“Kampeni hii ya Tusua Mapene bado inaendelea unachotakiwa ni kutumia mtandao wa Vodacom na kuandika neno V tuma kwenye namba 15544 au nenda kwenye MPesa ukitumia ile namba yake ya kawaida *150*00# kisha nenda namba 3 ambapo pale unanunua bando lakini ukiangalia pale utakuta namba 7 fungua pale utaweza kununua tiketi yako ya siku, ya wiki au mwezi halafu Unatusua Mapene unasubiri tu kama unaweza kujipatia shilingi milioni ishirini.

“Nawakaribisha wateja wote ambao bado hawajajiunga wa Vodacom waje kwenye na mtandao wetu kwa maana sisi ni zaidi ya mtandao”. Alimaliza kusema Mkuu wa Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Birgita Shirima.

Leave A Reply