VODACOM YAKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA VPL 2017/18
Usiku wa June 23, 2018 ulishuhudia utoaji wa Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/18 kwa washiriki na wadau waliofanya vizuri katika ligi hiyo ikiwa ni pamoja na makocha, wachezaji na kadhalika.
Tuzo ya Mfungaji Bora ilienda kwa Emmanuel Okwi wa Simba mwenye mabao 17 ambaye alituzwa Sh milioni tatu. Kwa timu zilizoshika nafasi mbalimbali, nafasi ya nne ilichukuliwa na Prisons ya Mbeya ambayo ilipata Sh mil. 27, Yanga ya tatu ilipata mil. 34, Azam ya pili ilipata mil. 48 na mabingwa Simba mil. 96.
PICHA: RICHARD BUKOS | GPL
Comments are closed.