The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yasaidia Kituo Cha Watoto Yatima Cha Sifa Mkoani Pwani

Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Sifa Gifty Makola akikabidhiwa msaada wa madaftari na Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (kushoto).
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania PCL kitengo cha biashara, Julius Kastabu (kulia) akimkabidhi msaada wa ndoo ya mafuta ya kupikia mkurugenzi wa Sifa Group Foundation Children Center.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Sifa Group Foundation.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc, pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Sifa Group Foundation Children Center wakiangalia mtanange wa kucheza boa la kuchibwa chini baina ya meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (kushoto) na Moses Bakari, ambaye aliibuka mshindi.
Wafanyakazi wa kitengo cha biashara cha kampuni ya Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na taasisi ya kuhudumia masuala ya jamii ya Vodacom Tanzania Foundation wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali ya shule na mengineyo kwa ajili ya kusaidia watoto wanaolelewa katika kituo cha Sifa Group Foundation Children Center, kilichopo Ubafu Vikawe, kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha. 
Mbali na msaada huo wa mahitaji yenye thamani ya shilingi milioni 18, taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imewezesha kujenga na kufunga tenki la maji safi katika kituo hicho.

Comments are closed.