Vodacom Yashirikiana Na TECNO Uzinduzi Camon 20
Meneja Bidhaa za Internet kutoka Vodacom, Samweli Mlole (katikati) na maofisa wa TECNO wakionyesha simu hiyo.
Dar es Salaam 20 Mei 2023: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya TECNO imefanya uzinduzi wa leo simu janja mpya aina ya TECNO Camon 20 yenye ubora wa hali ya juu ambapo uzinduzi huo umefanyika mapema leo Mei, 20, 2023 Golden Tulip, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati uzinduzi wa simu hiyo, Meneja Bidhaa za Internet wa Vodacom Tanzania, Samweli Mlole amesema kuwa wanafuraha kubwa kwa kuwa Kampuni ya TECNO ambayo imewaamini na kuendelea kufurahia kufanya nao kazi.
“Kama mnavyojua sisi Vodacom ni zaidi ya mtandao kwa sababu tumevuka kufanya shughuli zetu kama mtandao wa simu tu wa kawaida na tumeboresha huduma zetu na bidhaa zetu kwa hali ya juu.
“Hivyo kuweza kuonekana na kufanya shughuli zetu kuwa zaidi ya mtandao hivyo basi leo tunajumuika pamoja na ndugu zetu TECNO Tanzania kuwatelea simu bora yenye uwezo kwa sifa ambazo zimetajwa na ndugu zetu wa TECNO,” amesema Mlole.