The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yazindua Huduma ya Bima ya Afya Kupitia Mfumo wa M-Pesa

0
Mkurugenzi wa Mpesa , Epimack Mbeteni akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima “Linda afya na VodaBima” uliofanyika jijini Dar es salaam, Vodacom kwa kushirikiana na kampuni za Jubilee Insurance ,Mo Assurance pamoja na Milvik Tanzania watatoa huduma za bima ya afya inayolenga kutumia mfumo wa kidijitali katika utoaji wa huduma za afya jumuishi nchini.

 

 

13 Mei 2022, Vodacom Tanzania Plc, kampuni inayoongoza kwa huduma za teknolojia na mawasiliano, nchini leo imetangaza ushirikiano na Milvik kutoa huduma za bima ya afya kutoka Jubilee Insurance na Mo Assurance inayolenga kutumia dijitali katika utoaji wa huduma za afya jumuishi.

Meneja Masoko wa M-Pesa, Noel Mazoya akizungumza kabla ya uzinduzi wa huduma ya VodaBima “Linda afya na VodaBima” kwenye ofisi za makao makuu ya Vodacom jijini Dar es salaam.

 

 

Upanuzi huu unakuja baada ya kampuni hiyo kufanikiwa kwa bidhaa zake za bima ya magari kupitia Voda Bima ambayo inatoa huduma za bima kubwa na ndogo kwa ushirikiano na kampuni 10 zinazotoa huduma za bima wanaoongoza nchini, jambo ambalo litawezesha Watanzania kupata huduma muhimu za afya.

Mkurugenzi wa M-pesa , Epimack Mbeteni (wa pili kulia) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Insurance, Dinpankar Acharya (kushoto), Meneja wa Utekelezaji Sheria na Kushughulikia Malalamiko (TIRA), Okoka Mgavilenzi (watatu kulia), Afisa Bima Mkuu Mo Assurance, Pamela Ndosi (wa pili kushoto), mkuu wa Kitengo cha Mauzo Milvik, Ismail Simanga (Watatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja ya uzinduzi rasmi wa huduma ya VodaBima “Linda afya na VodaBima”

 

 

Vifurushi vya bima ya Afya kutoka kwa washirika hawa vitaweza kuwafikia kwa urahisi wateja na vinapatikana kwenye huduma za Vodacom M-Pesa.

Vifurushi hivyo ni vya bei nafuu na vinatarajiwa kurahisisha mchakato wa matibabu ya afya nchini.

Vifurushi vilivyoanzishwa ni pamoja na malipo ya wagonjwa wanaolazwa hospitalini, ajali, maisha na bidhaa iliyounganishwa (FarajaYangu) ambayo hutoa faida na kwa wengine, kwakuwa uhusisha watu wazima na watoto na hutofautiana kwa bei kulingana na umri wao na virufushi maalum.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Vodacom M-Pesa,Epimack Mbeteni alisema, “Tuna furaha kubwa leo kuweza kutangaza maendeleo haya muhimu katika utoaji wa bima kwa Watanzania.

Vodacom Tanzania imeweka mkazo mkubwa kwenye afya kama kichocheo kikuu cha shughuli zetu zinazoongozwa na malengo.

 

Huduma ya afya ni hitaji la msingi kwa Watanzania wote na tunaamini inapaswa kupatikana kwa urahisi kwa wote, hivyo ushirikiano wetu na Milvik, Jubilee na Mo assurance utasaidia kufungua hitajihili.”

Vodacom imekuwa ikishiriki kikamilifu katika utoaji wa huduma za afya nchini kwa miaka mingi, imeweza kutoa msaada katika maeneo tofauti kama vile matibabu ya fistula ya uzazi, msaada na matibabu kwa watoto wachanga na familiazao.

 

Mwezi uliopita, kampuni pia ilifanikiwa kuzindua mpango wake wa m-mama kusaidia wanawake wajawazito wanaopata dharura wakati wakujifungua.

 

Vifurushi hivi vya bima ya afya vinakuja kufuatia mapokezi chanya ya bima ya magari iliyoanzishwa mapema mwaka huu kwa ushirikiano na kampuni 10 za bima ambapo sasa Watanzania watafurahia urahisi wa kununua bima kutoka eneo lolote nchini bila adha ya kutembelea ofisi za wakala yeyote wa bima.

Vodacom Tanzania PLC inaendelea kufanyakazi ya kutoa suluhu za kibunifu zaidi kwa wateja wake, juhudi ambazo hivi karibuni zimeiwezesha kupata tuzo ya mtoa huduma bora ya mtandao wa simu kutoka Tume ya TEHAMA nchini.

Kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Meneja Utekelezaji Sheria na kushughulikia malalamiko (TIRA), Okoka Mgavilenzi alisema serikali inahimiza matumizi ya teknolojia katika kupata na kutoa huduma muhimu za kidijitali ikiwemo bima. “Tunaipongeza Vodacom Tanzania kwa kuja na ubunifu huu na kuchukua hatua kubwa ya kuongeza watoa huduma wengi wa bima kwenye mtandao wa kidijitali wa Voda Bima ambao tunaamini utaongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji na matumizi ya huduma ya bima nchini hasa katika eneo la afya ambayo umezindua leo,” alisema Mgavilenzi.

 

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Milvik, Ismail Simanga alisema tukio hilo lilikuwa hatua kubwa sana ambayo itashuhudia afya ya familia ikilindwa vyema na bima bora ya afya.

 

“Afya na usalama wa familia yako inamaanisha ulimwengu kwako. Tunaelewa na tunataka kukusaidia kuwalinda wapendwa wako dhidi ya hali zilizo nje ya uwezowako”.

 

Kupitia jukwaa la MPesa watanzania wataweza kupata bima zetu popote pale walipo bila tabu yoyote.

 

 

 

Leave A Reply