Kartra

Vuai Nahodha Achukua Fomu Urais Zanzibar

WAZIRI Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nahodha ambaye alikuwa Waziri Kiongozi kuanzia mwaka 2000 – 2010 amefika katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui mapema asubuhi leo na kuchukua fomu ya Urais.

Wanachama wengine waliochukua fomu ni Mbwana Bakari Juma, Ali Abeid Karume, Mbwana Yahya Mwinyi, Dkt. Hussein Mwinyi na Omar Sheha Mussa.

 

SHAMSI VUAI NAHODHA

Umri: 59yrs

Uzoefu:

-Mbunge Mwera

-Mbunge Mwanakwerekwe

-Katibu Kiongozi Zanzibar

-Mbunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

-Waziri Mambo ya ndani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

-Waziri wa ulinzi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Toa comment