The House of Favourite Newspapers

Vyakula Hatari Kwa Afya Yako

0

CHAKULA bora ni muhimu kwa afya na furaha yako, bila chakula bora, hakuna raha katika maisha yako hapa duniani. Katika mada yetu ya leo tunaangalia vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine hupunguza uhai kwa binadamu, hivi ni vyakula ambavyo vinaweza kukufanya ukapata magonjwa usiyotarajia, mfano saratani (cancer), kisukari na magonjwa ya shinikizo la damu au moyo.

 

Upo usemi unasema ‘tunakula ili tuishi, si tunaishi ili tule’. Hapa maana yake ni kwamba wale wanaopenda kuishi ili kula hufakamia chochote ili mradi kiwe chakula, tofauti na wale wanaoishi ili kula maana hujali zaidi afya zao kwanza kuliko njaa, utamu au mvuto wa chakula. Kuwa na uwezo wa kupata vyakula mbalimbali vitamu huwa haiwezi kumfanya mtu makini asahau vitu muhimu kwa afya yake.

 

VYAKULA VYA KUSINDIKA

Vyakula vingi vya kusindika ambavyo hutumiwa na watu wenye uwezo kifedha huweza kukaa muda mrefu kwa kutumia dawa, sukari, mafuta na chumvi kwa kiwango kikubwa sana, hivyo kuwa hatari kwa mtumiaji.
Vyakula vilivyohifadhiwa kwenye makopo au chupa hakuna hata kimoja kinachokusaidia mwilini bali hukuletea madhara zaidi. Hivyo, ili kuwa na afya bora, unashauriwa kupunguza kula vyakula vya kusindika na pendelea kula vyakula asilia, hasa mboga za majani na matunda.

 

SODA

Mara nyingi vinywaji visivyo na vilevi vimekuwa havimo kwenye orodha ya vitu visivyo vya afya. Lakini ukweli ni kwamba, vinywaji vingi sana vinavyouzwa viwandani si vizuri kwa afya yako. Mfano mzuri ni soda. Soda ina kiwango kikubwa sana cha sukari. Madaktari wengi wameonyesha kuwa madhara ya soda hayatofautiani na madhara ya
kuvuta sigara. Kiwango cha sukari na dawa zilizomo kwenye soda humfanya mtu kuzeeka na kumletea madhara ya magonjwa kama kisukari kwa muda mfupi.

 

NYAMA NYEKUNDU

 

Kwa muda mrefu sana nyama nyekundu imegundulika kuwa chanzo cha magonjwa sugu kama magonjwa ya moyo kutokana na mafuta yake kuganda na kuziba mishipa ya damu na husababisha saratani. Nyama siyo nzuri kwa afya sababu husababisha kuongezeka kwa uzito kupita kiasi kama ikiliwa kwa kiwango kikubwa sana.

 

POMBE

Pombe haihitaji maelezo mengi. Kila mtu anafahamu madhara yake ya muda mfupi, ambayo huleta matokeo mabaya zaidi kwa wale watumiaji wa muda mrefu. Pombe, inayonywewa kwa kiwango kikubwa kila mara,

 

CHAKULA

hupunguza sana urefu wa maisha sababu huharibu chembechembe muhimu mwilini hivyo kuufanya mwili kukosa kinga, na kudhoofika. Ikifikia kiwango hiki inakuwa rahisi kupata magonjwa, na kutoweza kuwa na kinga ya kutosha mwilini.

ZINGATIA HAYA

Ni vizuri kujali afya, hivyo basi, ni vizuri ukizingatia haya machache: Pendelea vyakula asilia hasa mboga za majani na nafaka bora, tumia matunda zaidi, ni bora kuliko juisi inayoongezwa sukari au soda za kununua, pendelea kula chakula nyumbani kilichoandaliwa vizuri kwa afya.

 

Usitumie kilevi, kama huwezi, basi kunywa kiasi, ili usiharibu afya yako. Pendelea kuangalia kiwango cha virutubisho kwenye kila chakula unachokula na hakikisha unakunywa maji kwa kiwango kinachotakiwa, acha kula vyakula vyenye mafuta mengi, hasa ya wanyama, kwani husababisha matatizo ya kuziba mirija ya damu..

Makala haya imendikwa na Mtaalamu wa Lishe, Abdallah Mandai kwa ushauri piga 0717 961795, 0754 391 743.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply