The House of Favourite Newspapers

Vyakula Vinavyosaidia Kuongeza Nguvu Za Kiume-2

0

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo, utakubaliana na mimi kwamba, wanaume wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume na ndiyo maana wiki iliyopita nilianza kuzungumzia mada hii inayohusu vyakula vinavyoweza kusaidia kuongeza nguvu za kiume.

Wiki hii nitaimalizia makala hii ili wiki ijayo nianze mada nyingine Madini pia ni muhimu kwa afya ya nguvu za kiume, madini huwa yanatoka ardhini, madini yanayohitajika mwilini ni mengi lakini yanayohitajika katika kuimarisha nguvu za kiume ni selenium, zink na potasium kwa kiasi kidogo. Madini ya potasium husaidia kuondoa uchovu wa mwili au fatique au hutamkwa fatiki, kutokana na shuruba mbalimbali za kutwa nzima.

Uchovu huu pia huchangia kupunguza kasi ya ufanyaji wa tendo la ndoa. Mwanaume mwenye upungufu wa madini ya potasium mwilini huchoka sana baada ya kumaliza tendo la ndoa na huhisi mwili unauma. Madini hupatikana katika vyakula vya jamii ya mizizi na baadhi ya matunda kama tutakavyokuja kuona.

AINA ZA VYAKULA VYENYE MADINI YANAYOONGEZA NGUVU ZA KIUME

Vyakula hivi ni vya asili na hupatikana na kuliwa katika uasili wake.

MIHOGO; mihogo ina kiwango kikubwa cha madini ya Zink na Potasium na ni bora zaidi ikitafunwa mibichi, inapopikwa kiwango cha madini haya hupungua, jamii zote za vyakula vya mizizi kama karoti, viazi aina zote na magimbi yana madini haya kwa wingi endapo utatafuna kwa kiasi. Ulaji wake katika hali ya ubichi ni wa kiasi kidogo wala huhitaji kula lundo la vyakula hivi, lakini angalau kwa kiasi kidogo kila siku kinatosha.

NDIZI; Ndizi mbivu ni muhimu sana katika suala hili, ndizi mbivu zina
madini ya selenium na potasium ambayo ni msaada mkubwa katika kuondoa uchovu wa mwili na kuimarisha nguvu za kiume. Ulaji wa wastani kila baada ya mlo husaidia.

SHARUBATI; Hii ni aina yoyote ya juisi itokanayo na matunda asilia mfano maji ya madafu, kukamua machungwa, miwa, nanasi, maembe na mengineyo husaidia kuongeza madini ya potasium na kuondoa uchovu wa mwili, hivyo husaidia kuboresha uwezo wa kufanya tendo la ndoa.

USHAURI; Vyakula vyote tulivyoelezea kuanzia vile vyenye vitamini hadi hivi vyenye madini ni vema vikaliwa katika utaratibu maalumu, vyakula hivi sio tiba bali husaidiana na tiba. Hivyo basi kama una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni vizuri umuone daktari katika hospitali ili ufanyiwe uchunguzi na kupatiwa matibabu sahihi.

H Baba, Flora Mvungi Utajiri Nje Nje!! Mtoto Wao Alamba Dili Nono


Leave A Reply