Vyakula vinavyotibu fangasi wa mdomoni

Mara nyingi vyakula tunavyokula huwa na faida mwilini lakini vingine huwa na madhara fulani ambayo sisi huwa hatuyajui hasa kama unashambuliwa na ugonjwa fulani.

Leo nimeona niliongelee hili kwenye safu hii maalum ya kukujuza jinsi ulavyo ndiyo matokeo ya baadaye.

Wapo wengi wanaosumbuliwa na suala la fangasi wa mdomoni lakini hawajui tiba wala sababu ya wao kupata ugonjwa huo.

Mara nyingi ugonjwa huu huwapata watoto wanaonyonya ingawa wao ni kawaida na mama huelezwa hospitali jinsi ya kufanya.

Ugonjwa huu ukitokea kwa wakubwa huwa si jambo la kawaida kwani husababisha mtu kujihisi vibaya kwa sababu wakati mwingine unaweza kujikuta ukinuka mdomo bila kujua tatizo na utando mweupe unaweza kukutoka, hii ni dalili kwamba umepata maambukizi.

Ni rahisi pia kuunguzwa na chakula hata kama hakikustahili kukuunguza kwa kiwango kikubwa, kwani ngozi ya ulimi inakuwa imeshashambuliwa na bakteria wa fangasi.

Vyakula vinavyosababisha fangasi:

Vyakula hivyo ni karanga, mayai, maziwa ya kawaida, maziwa mgando, yougurt ya baridi, vinywaji vyote nyenye kafeni kama vile kahawa, chai, chokoleti nk.

Vingine ni soseji nyama nyekundu, mayonnaise, salad, pia vyakula vyote vya baharini. Hivi ni vichache tunavyopendelea kula, kama wewe una tatizo la fangasi wa mdomoni nakusihi kuacha au kula kwa uchache vyakula hivyo wakati unatibu ugonjwa huu.

Vyakula tiba

Mdalasini ‘Cinnamon’:

Hiki ni kiungo kinatajwa kutibu moja kwa moja ugonywa huu, kwani kina uwezo wa kupigana na bakteria wanaoshambulia na wanaosababisha fangasi.

Jinsi mdalasini unavyoweza kutibu kama unapendelea kunywa yougurt, chukua unga wa mdalasini changanya kwenye yougurt yako kisha kunywa, pia unaweza kutumia chai ya mdalasini mara kwa mara.

Kama huwezi kuchanganya kwenye chai unaweza kuulamba unga wake kwenye asali asubuhi na jioni.

Majani ya mzaituni:

Majani ya mzaituni ni tiba kabisa yenye uwezo wa kuondoa fangasi.

Jinsi yanavyotibu:

Pika chai kisha kiungo chako kiwe majani ya mzaituni, unaweza kuweka majani mawili mpaka matatu kwenye chai yako au ukipata majani ambayo yameshaandaliwa kama majani ya chai ni vizuri kwani yapo yanauzwa kwenye maduka makubwa ya vyakula. Kunywa chai kama tiba kwa siku mbili.

Mafuta ya nazi:

Mafuta ya nazi ni mazuri kama tiba. Hakikisha kwenye kila mlo wako unachanganya kijiko kimoja cha chai kama unao uwezo wa kupata mafuta hayo unaweza kuyafanya tiba ukatumia mafuta ya nazi ya ndani ‘Virgin coconut’ vijiko vitatu kwa siku.


Loading...

Toa comment