The House of Favourite Newspapers

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

0

Kati ya wanaume watatu, mmoja ana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini.
Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi.
Ili kupata suluhisho la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia dawa hizo zenye nguvu. Vyakula ni suluhisho pekee na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.

Sababu za kukosa nguvu za kiume
Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au madawa, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kutokana na chakula unachokula. Je, wewe unakula chakula bora ili kulinda unyumba wako?

Vitu vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
– Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
– Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
– Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.

1. Blueberry
Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, yana virutubisho vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndiyo kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimili mapenzi kwa muda mrefu zaidi.

Soma pia: Njia 7 za kuongeza uzito
2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndiyo kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters).
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini ya zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya Testosterone, manii. Uwingi wa uzalishwaji wa Testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi husababisha hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi) na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.

4. Karanga.
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

5. Vitunguu saumu
Kitunguu saumu kina Allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

Soma pia: Jinsi afya ilivyo muhimu kwako
6. Ndizi
Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, hamu ya mapenzi (libido).

7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwa sababu ina viambato vya Phenylethylamine na Alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachosababisha kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na Alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.

Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa.
Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.
Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako.
Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea.

Leave A Reply