The House of Favourite Newspapers

VYAMA 15 VYA SIASA VYATOA TAMKO KUHUSU MUSWADA WA SIASA (Picha +Video)

Vyama 15 vya siasa nchini kupitia viongozi wake wakuu, leo Desemba 09, 2018, vimekutana na kutoa tamko la pamoja kuhusiana na mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa uliowasilishwa hivi karibuni na serikali bungeni wakati wa mkutano wa 13 wa bunge la 11 jijini Dodoma.

Vyama vinavyoshiriki mkutano huu ni ACT, CUF, UPDP, DP, CCK, CHADEMA, CHAUMA, NCCR, NLD na ADC.

Hashim Rungwe

Kiongozi wa CHAUMA, Hashimu Rungwe amesema muswada huo unalenga kuwapokonya wanasiasa uhuru wa kufanya shughuli za kisiasa na kuwaomba Watanzania wawaunge mkono viongozi hao kuzuia muswada huo usipitishwe na kuwa sheria kwa sababu unakiuka katiba ya nchi.

 

Naye Salum Mwalimu wa Chadema, amesema muswada huo una lengo la kuumaliza upinzani kwa kuwanyima wanasiasa haki yao ya kikatiba ya kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kisiasa na kuzungumza na wanachama wao.

Kwa upande wake, Zitto Kabwe amesema muswada huo unampa mamlaka makubwa msajili wa vyama vya siasa nchini, wa kuingilia shughuli za vyama vya siasa, hali ambayo amesema ni kinyume na katiba ya nchi, akaongeza kwamba Watanzania wanaoitakia mema nchi, wanapaswa kuwaunga mkono wanasiasa hao kuukataa muswada huo.

 

Comments are closed.