VYAMA NANE VYA UPINZANI VYAFUNGUA KESI DHIDI YA SERIKALI – VIDEO

Vyama nane vya Siasa nchini ikiwemo CHADEMA, CHAUMA, ACT WAZALENDO, DEMOCRATIC PARTY, CCK, UPDP vimeungana na kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kupinga matumizi ya Sheria ya vyama Vya Siasa ambayo vimedai kuwa inakandamiza misingi ya demokrasia.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema katika kesi yao wameomba mahakama ya Afrika Mashariki kutoa zuio la matumizi ya Sheria hiyo mpaka kesi yao ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo.

 

Loading...

Toa comment