The House of Favourite Newspapers

Vyama vvya Upinzani kuazisha upya kesi ya kumuondoa madarakani Rais Cyril Ramaphos

Rais Cyril Ramaphosa

Mahakama ya Kikatiba ya Afrika Kusini imesema Alhamisi mwezi ujao itasikiliza kesi iliyowasilishwa na Vyama viwili vya Upinzani kuanzisha upya kesi ya kumuondoa madarakani Rais Cyril Ramaphosa kufuatia kashfa ya zaidi ya Dola 500,000 ambazo zilifichwa kwenye kochi na kisha kuibiwa.

Ramaphosa aliepuka kura ya kumuondoa madarakani mwaka 2022 wakati chama chake, African National Congress (ANC) kilitumia wingi wa kura bungeni kuzuia hoja, hata baada ya ripoti huru kuibua maswali kuhusu mwenendo wake na kupendekeza uchunguzi kamili ufanyike.

Chama cha ANC tangu wakati huo kimeunganishwa na vyama vingine tisa katika muungano mpana wa kutawala Afrika Kusini, na kutuliza baadhi ya ukosoaji uliotolewa kwa Ramaphosa kuhusu kashfa hiyo.

Hata hivyo, vyama viwili ambavyo si sehemu ya serikali ya umoja wa kitaifa, Economic Freedom Fighters, chama cha mrengo mkali wa kushoto na Movement for the Transformation of Africa, vimewasilisha hati katika mahakama ya juu zaidi ya nchi hiyo, vikidai kuwa bunge limeshindwa kutekeleza sheria,kutimiza wajibu wake wa kikatiba katika kumwajibisha Rais.

UPDATES: VIFO vya AJALI ya BOTI ILIYOZAMA CONGO VYAONGEZEKA HADI 78 – ILIKUWA na ABIRIA 278…