The House of Favourite Newspapers

Wa Moyoni Wengi Wapo Kwa Wasio wa Moyoni

0

Celebrity-Couples-Pictures-Kissing-PDA-Instagram

MPENZI msomaji nakukaribisha katika siku nyingine mwanana ya Jumanne ambayo tumeifikia kwa kudura za Mwenyezi Mungu. Tunakutana tena katika kujadili namna maisha ya kawaida na mapenzi yanavyoenda.

Mada yangu ya leo itazungumzia namna ambavyo mtu anakuwa amemuweka mpenzi wake moyoni kwa kumjali, kumthamini, kumpenda, kumnyenyekea na namna yoyote ile ilimradi tu ni yenye kuonesha kuwa kweli ana upendo wa dhati kwa mpenzi wake huyo.

Lakini cha ajabu, bila kujua kuwa anayempenda na kumthamini wala hajamuweka kabisa moyoni mwake bali na yeye amemuweka moyoni mtu mwingine kabisaaa!

Mapenzi ya ajabu
Ama kweli mapenzi ni kitu cha ajabu sana, nilichokibaini katika uchunguzi mfupi nilioufanya nimebaini kuwa wapenzi walio na mapenzi ya dhati kwa wapenzi wao, kiukweli wapenzi wao wengi huwa hawana mapenzi ya dhati kwao kama wanavyodhani bali wanaowapenda wanamapenzi na watu wengine.

Ushahidi
Ninaamini ulishawahi kukutana na kisanga cha jamaa au mdada kumlilia na kumbembeleza mpenzi wake tena hata kwa kumpigia magoti na kutoa machozi lakini wakati huo anayebembelezwa wala hajali, wala ashituki kuwa anapendwa kiasi gani na ndiyo maana analiliwa, anapigiwa magoti anatumiwa wazee na viongozi wa kidini ili kuja kumuomba amsamehe mwenza wake lakini bado mtu huyo anakataa.

Unajua anakataa kwa nini anakuwa hajamuweka moyoni kama wewe ulivyomuweka ila yeye naye kuna mtu mwingine kamuweka moyoni mwake si ajabu hata yeye huwa analia na kupiga magoti kama ulivyomfanyia wewe, huwa anafanyiwa vihoja pengine zaidi ya anavyokufanyia lakini kwa sababu ndiyo kamuweka moyoni anavumilia.

Nini maana yake?
Wa moyoni wengi wapo kwa wasio wa moyoni, kuna mtu unampenda sana ila yeye hakupendi kama ambavyo wewe unatamani kumfanyia, kumlea na kadhalika kumbe na yeye kuna sehemu ndiko anakopenda lakini pia hata yeye nako huko hapendwi kama unavyompenda wewe.
Hapo ndipo haswaaa! Naposhawishika kusema kuwa ama kweli mapenzi ni mchezo wa ajabu sana.
Ila kikubwa hapa ni kuzidi kumuomba Mungu akuongoze kuwa waaminifu na kujitahidi kumpenda yule anayekupenda ili kudumisha uhusiano wako.

Leave A Reply