BALAA limewakumba Waafrika walioko nchini China wakidaiwa kuwa wameingiza nchini humo virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa unaojulikana kama Covid-19 ambao umeikumba sehemu kubwa ya dunia na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.
Hivi sasa Waafrika wanafukuzwa kutoka majumbani mwao na mahotelini wanakoishi kwa madai kwamba wao ndiyo walioingiza virusi hivyo nchini China.
Waafrika walio katika majimbo ya Guangdon na Fujian wanakabiliwa na balaa hilo la usumbufu ambapo serikali pia inatumika kuwaondoa katika makazi yao.
Tobenna Victor, mwanafunzi kutoka Nigeria anasema, “Jamaa wanatuambia eti tuna virusi hivyo. Pamoja na kuwalipa kodi za pango bado wanatufukuza katika nyumba zao.”
Naye Lunde Okulunge Isidore, mfanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (D.R.C) anasema wanawekwa kwenye karantini kwa nguvu bila hata kufanyiwa uchunguzi wa afya zao.
“Watu kutoka nje ya China hususani watu weusi hawaruhusiwi kuingia kwenye maduka makubwa, migahawa na kwenye hospitali,” anasema Isidore.
Mikutano ya Waafrika walioko Guangzhou nchini humo imekuwa ikifanyika kuhusu suala hilo lakini bado Waafrika wamekuwa wakijikuta wakihangaishwa.
Matukio hayo ya kunyanyaswa watu weusi yaameibua hisia za ubaguzi nchini humo mbali na kwamba matukio yenye kuhusiana na mazingira hayo huwa hayazungumzwi hadharani.
Pia kumekuwepo na hisia kwamba pamoja na China kukubalika barani Afrika katika kuwekeza kwake kiuchumi barani humo, bado Waafrika wakiwa nchini China wanakuwa wanakabiliwa na manyanyaso kama hayo nchini humo.
Katika kusisitiza msimamo huo dhidi ya Waafrika mamlaka za China zimetoa maelekezo ya kuwafanyia uchunguzi wa afya zao Waafrika katika maeneo wanayokaa kuhusiana na ugonjwa huo ili kuondoa hisia hizo za ubaguzi.
VIDEO: While the world has adopted various measures to combat #Coronavirus, Chinese authorities are beginning to eject Africans from their homes and hotels over claims that they were importing the virus into the country.#COVID19 pic.twitter.com/x78SZhhSMO
— Sahara Reporters (@SaharaReporters) April 7, 2020
Mpaka sasa, watu 1,703,147 wamripotiwa kuambukizwa Coronavirus duniani kote, huku vifo vilivyotokana na ugonjwa huo vikiwa ni 102,864, na waliopona ni 377,813.
Ikumbukwe kuwa siku za nyuma, China ndiyo ilionekana kuwa na vifo vingi zaidi kutokana na covid – 19 lakini mpaka sasa, Italy ndiyo nchi inayoongoza kwa vifo ikiwa na 18,849, Marekani ya pili ambayo ina vifo 18,761, Hispania ina vifo 16,081, Ufaransa ina vifo 13,197, Uingereza ina vifo 8,958, Irani ina vifo 4,232 na China ina vifo 3,339.
Marekani ndiyo nchi inaongoza kwa maambukizi ikiwa na watu 503,177 huku china ikishika nafasi ya sita kwa kuwa na wagonjwa 81,953.
China imekuwa miongoni mwa nchi ambazo zimefanikiwa kudhibiti kwa kiwango kikubwa mlipuko wa ugonjwa huo mpaka sasa na hivi juzi ilitoa ruhusa kwa mamilioni ya Wakaazi wa Jimbo la Wuhan waliokuwa wamezuiliwa kutoka nje ya Jimbo hilo kwa muda mrefu kutokana na hofu ya maambukizi ya Covid -1 9.
Source – Sahara Reporters




