Waandishi wa Habari Wanawake Wapewa Semina ya Kujilinda Wawapo Kazini
WAANDISHI wa habari wanawake wamepewa semina juu ya kujilinda wakati wa utekelezaji wa majukumu yao katika semina iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika semina hiyo, Mwalimu Neema Rugaimukamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amewataka waandishi wa habari wanawake kujua haki zao wanapokuwa kazini ili waweze kuwa na ujasiri na kusimama na kujitetea na kutokukubali kupewa vitu rahisi kwani wanawake wanao uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi kama wanaume.
Kwa upande wake, Afisa Jinsia na Habari kutoka Tamwa, Edina Salila ametoa mapendekezo kuwa na usawa katika utendaji kazi ndani ya vyombo vya habari na kuheshimika pamoja na kupewa nafasi kulingana na uwezo.