The House of Favourite Newspapers

Waandishi Wavamiwa Na Kujeruhiwa Kwa Mikuki Ngorongoro, Hali Zao Mbaya – Video

0

Zaidi ya vijana 200 wa jamii Ngorongoro, Mkoani Arusha wamewavamia na kuwajeruhi waandishi wa habari na mkalimani aliyeambatana nao. Waandishi hao wamekuwa wilayani humo wakipata uelewa wa kwa nini Serikali inashauri wahame kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi hiyo kwenda Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Waandishi waliojeruhiwa ni pamoja na Ferdinand Shayo wa ITV, Denis Msacky (mwandishi wa kujitegemea), Habib Mchange (Jamvi la Habari), mkazi mwingine wa Ngorongoro, Lengai Ngoishie.

Vijana hao walikuwa wamebeba mapanga, mikuki, sime na mishale. Wakati tukio hilo linatokea Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Oleshangai, alikuwepo eneo la tukio na baada ya vijana hao kuvamia na kujeruhi alioondoka eneo hilo.

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwala amesema anatuma askari kufika eneo hilo la tukio.

Leave A Reply