The House of Favourite Newspapers

Waangalizi wa EU wakosoa uchaguzi Uganda

0

burundi (2)Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU).

Waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) wamekosoa namna ambavyo uchaguzi mkuu wa Uganda ulievyoendeshwa na kusema mabadiliko makubwa yanahitajika.

Wakizungumza na wanahabari nchini humo, viongozi wa ujumbe kutoka Muungano wa Ulaya wamesema kulitokea kasoro nyingi kuhusiana na shughuli nzima ya uchaguzi.

burundi (1)Dkt Besigye alivyokamatwa majuzi

Mwangalizi mkuu wa Umoja wa Ulaya, Eduard Kukan amewaambia wanahabari kwamba ni dhahiri Tume ya Uchaguzi ya Uganda haikujifunza kutokana na mapendekezo yaliyotolewa umoja hu baada ya uchaguzi mkuu wa 2011.

Aidha, amesema haikuwa haki kufunga uandikishwaji wa wapiga kura Mei mwaka jana, huku akisema hatua hiyo imewanyima haki ya kupiga kura raia waliotimiza umri wa miaka 18 baada ya tarehe hiyo.

uganda (1)

“Tume haina uwazi na wadau hawana imani nayo. Tume haina uwazi katika kufanya maamuzi na katika kuwafahamisha wapiga kura kwa wakati na kwa ufasaha,” alisema Kukan.

Bw Kukan akaendelea kueleza kuwa, kucheleweshwa kwa karatasi na vifaa vya kupigia kura pamoja na kuchelewa kuanza kwa upigaji kura siku ya uchaguzi kuliathiri imani ya watu katika zoezi hilo.

Ugandans queue up to cast their votes at a polling station that had not received any voting materials on election day, in Ggabe, near Kampala, in Uganda Friday, Feb. 19, 2016. Police in Uganda arrested opposition leader Kizza Besigye at his party's headquarters Friday after heavily armed police surrounded the building and fired tear gas and stun grenades at his supporters who took to the streets. (AP Photo/Ben Curtis)Ameshutumu pia kukamatwa na kuzuiliwa kwa kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye ambaye pia ni mgombea urais kwenye uchaguzi huo, pamoja na kufungwa kwa mitandao ya kijamii. Dkt Besigye alikamatwa na polisi mara tatu ndaniya wiki hii.

Mwangalizi Mkuu wa Bunge la Ulaya, Jo Leinen kwa upande wake amesema wagombea wote hawakupewa nafasi sawa katika vyombo vya habari na wanasiasa pamoja na raia waliounga mkono upinzani walipatwa na misukosuko kutoka kwenye vyombo vya usalama nchini humo.

Amesema pia kwamba fedha za serikali na chama lazima kutenganishwa. “Kuna mengi sana ambayo yanafaa kurekebishwa,” alisema Leinen.

Waangalizi wa Jumuiya ya Madola, wanaoongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, pia wameeleza kutoridhishwa kwao na baadhi ya mambo yaliyotokea wakati wa uchaguzi.

Ameshutumu kukamatwa na kuzuiliwa kwa Dkt Besigye akisema hatua hiyo iliongeza tu wasiwasi. Matokeo kamili ya uchaguzi wa urais yanatarajiwa kutangazwa kabla ya saa kumi alasiri leo.

Matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa yanaonyesha Rais Yoweri Museveni anaongoza akiwa na zaidi ya asilimia 60 ya kura dhidi ya Dkt Kizza Besigye aliye na asilimia 34 ya kura zilizohesabiwa.

Leave A Reply