The House of Favourite Newspapers

Waarabu Wa Yanga Waanza Vituko

Wachezaji wa USM Alger wakipongezana katika mechi ya kwanza na Yanga.

USM Algiers ambao wanacheza na Yanga kesho saa 1 usiku kwenye mechi ya kukamilisha ratiba kwa Yanga katika michuano ya Shirikisho, wametoa masharti kwa waandishi wa habari.

 

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema katika kikao chao na uongozi wa Yanga ambao ni wenyeji na USM Alger walikubal­iana kuwa timu hiyo itafanya ma­zoezi yake katika Uwanja wa Taifa saa moja kamili usiku.

 

Ndimbo alisema, muda waliotoa kwa waandishi ni dakika 15 pekee ambazo watatumia kuripoti kuanzia saa moja kamili hadi saa 1:15 na baada ya hapo watawatoa nje na wao kuendelea na program zao za mazoezi.

 

“Wameingia mapema leo (jana) asubuhi na tumefanikiwa kukaa kikao cha pamoja kwa maana ya uongozi wa TFF, Yanga na USM Al­ger ili kujadiliana taratibu muhimu, na katika kikao hicho kulikuwa na changamoto kidogo ambapo USM Alger hawakuhitaji mtu aingie uwanjani wakati wa mazoezi yao lakini tukawaomba watoe nusu saa kwa waandishi kwa ajili ya kuripoti lakini waligoma na kutoa dakika 15 pekee.

 

“Hatukutaka kubishana katika hilo, hivyo tuliamua kuheshimu utaratibu wao kwani kila timu ina misingi yake na hasa inaposafiri kama hivi, kubwa tumewataka wafanye wawezavyo ila wasivunje kanuni za mashindano tu kwani kufanya hivyo kunaweza kuwasaba­bisha kuadhibiwa.”

 

Waarabu hao wanatarajiwa ku­fanya mazoezi hayo leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa na Yanga wao walifanya jana usiku. Hata hivyo Yanga ipo kambini mkoani Morogoro na imepanga kurejea leo Jumamosi.

 

Wakati huohuo, Kocha wa USM Alger, Mfaransa, Thierry Froger, amesema kuwa wametua nchini kwa lengo la kupambana na kuon­doka na alama tatu ili waweze kuon­goza kundi lao.

 

“Tumekuja kupambana, kwetu huu ni mchezo muhimu ambao tunahitaji kupata ushindi ambao utatusaidia huko mbeleni na ku­weza kusonga mbele.

 

“Nafahamu timu zote zimejipanga kupambana ili kupata matokeo na mimi nitapambana na vijana wangu kuweza kukamilisha hili,” alisema Thierry.

Stori na Musa Mateja na Martha Mboma

Sababu za BOCCO, KAPOMBE, Kukosa Mechi ya Ngao ya Jamii!

Comments are closed.