The House of Favourite Newspapers

Waarabu Wamsaka Ajib Bongo

Mshambuliaji Ibrahim Ajib.

BAADA ya kuwa na mafanikio msimu huu ndani ya Yanga, mshambuliaji Ibrahim Ajib anatakiwa na timu kutoka Uarabuni.

 

Kijana huyo amekuwa ma­hiri msimu huu na hadi sasa ameshatoa pasi sita za mabao na kufunga mawili, akiwa ndiye mchezaji hatari zaidi kwa sasa kwenye ligi.

 

Yanga imecheza michezo sita kwenye ligi kuu huku wakishinda michezo mitano na kutoa sare moja huku Ajibu akiwa msaada kwenye mechi hizo.

 

Akizungumza na Champini Jumatano, Meneja wa Ajib, Athu­man Ajibu, alisema kuwa mcheza­ji huyo amepata ofa nyingi kutoka kwenye timu za Uarabuni.

 

“Kwa sasa nimekuwa nikiongea na wamiliki wa timu mbalimbali ambao wanamfuatilia Ajibu, wapo wale wa ndani ya nchi ambao nao kupitia mawakala wao nimeongea nao wakione­sha kukubali uwezo wa Ajibu ila nimeshindwa kuwakubalia kwa kuwa bado ni mali ya Yanga kwa sasa.

 

“Kuna timu tano, ambazo zimeleta ofa ikiwa ni pamoja na timu moja iliyopo Afrika Kusini na nyingine ipo Uarabuni, naamini kuwa anaweza kwenda kokote, aidha Afrika Kusini au Uar­abuni lakini kwa makubaliano na Yanga,” alisema meneja huyu ambaye ni ndugu wa mchezaji huyo.

 

Wakati huohuo, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye hakuwepo uwanjani Jumapili ambapo Ajib alifunga bao kali la kideo, amesema kuwa aliona mechi hiyo na bao alilofunga Ajibu ni zuri lakini wengi sana duniani wamefanya hivyo.

 

“Niliona ile mechi ya Yanga na Mbao hata bao lile ambalo alifunga Ajib nimeliona, ni zuri lakini sasa niko bize na timu ya taifa ya Congo, ila wachezaji wen­gi wamewahi kufunga hivyo hata huko Ulaya,” alisema Zahera.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka | Championi Jumatano

Comments are closed.