Waarabu wamvamia mwamuzi kisa bao la Okwi

Emmanuel Okwi na Chama wakishangilia.

MMOJA kati ya viongozi wa benchi la ufundi wa Js Saoura, jana Jumamosi alimvamia mwamuzi Joshua Bondo wakilalamikia bao lililofungwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.

Kiongozi huyo akiwa na kipa Khaled Boukacem walimzonga mwamuzi wakilalamikia bao lilofungwa dakika 45 kabla ya mapumziko.

 

Spoti Xtra limewashuhudia kipa na kiongozi huyo wakimzonga mwamuzi mara baada ya filimbi ya mapumziko hali iliyomfanya kocha wa Simba, Patrick Aussems kuingilia kati kabla ya kuja kwa maofisa wa CAF kuwaongezea ulinzi wakati wakitoka nje.

 

Lakini ulinzi huo haukuweza kusaidia kutokana na kipa huyo kuendelea kulalamika huku wakiwa wanaelekea vyumbani

STORI NA IBRAHIM MUSSA

Loading...

Toa comment