The House of Favourite Newspapers

Waasi Wa M23 Waeleza Kwamba Nia Yao ni Kuukamata Mji Mkuu wa Kinshasa

Kiongozi wa Muungano wa Waasi wa Congo River Alliance unaolijumuisha kundi la wapiganaji wa M23, Corneille Nangaa

Kiongozi wa Muungano wa Waasi wa Congo River Alliance unaolijumuisha kundi la wapiganaji wa M23 waliofanikiwa kuuteka Mji wa Goma, Corneille Nangaa amesema lengo lao siyo kuiteka Goma pekee bali wanaitaka Kinshasa ili kumuondoa madarakani Rais Felix Tshisekedi.

Kauli hiyo inakuja muda mfupi baada ya waasi wa M23 kuushikilia Uwanja wa Ndege wa Goma pamoja na maeneo mengine muhimu katika mji huo, huku risasi na mabomu vikiendelea kusikika usiku kucha.

Nangaa ambaye ni swahiba wa karibu wa Sultani Makenga, kiongozi wa wapiganaji wa M23, amenukuliwa akisema matatizo yanayokabili nchi hiyo yanatokana na uongozi mbovu wa serikali hivyo wataiteka Kinshasa ambayo ndiyo makao makuu ya serikali na kumuondoa Tshisekedi.

NUSRAT BULEMBO – “WANAWAKE WENGI WANA SHIDA ya AFYA ya AKILI – KUNGWI SIYO LAZIMA UFUNDISHE VIUNO”..