Waasi Wanaoungwa Mkono na Urusi Wadai Kudhibiti Kijiji cha Mashariki mwa Ukraine
VIKOSI vya Waasi wanaoungwa mkono na Urusi, vimechukua udhibiti kamili wa Kijiji cha Pisky kilicho nje kidogo ya Mji wa Donetsk Mashariki mwa Ukraine.
Moscow inatafuta udhibiti wa Donbas inayozungumza Kirusi kwa kiasi kikubwa, hii inajumuisha Mikoa ya Mashariki ya Luhansk na Donetsk ya nchi ya Ukraine.
Watu wa Mikoa hiyo kwa kiasi kikubwa wanaiunga mkono Urusi na wameshikilia maeneo mengi tangu mapema mwaka 2014.
Shirika la habari la Urusi TASS limeripoti likinukuu vikosi vinavyotaka kujitenga:
“Kijiji cha Pisky kipo chini ya udhibiti wetu, inaweza kusemwa kwa uhakika”
TASS ilimnukuu Llya Yemelyanov ambaye ni Naibu Kamanda wa wale wanaojiita wanamgambo wa watu wa Jamhuri ya Donetsky.
Pia Jeshi la Ukraine siku ya Alhamisi lilisema kwamba vikosi vya Urusi vimeishambulia Pisky angalau mara mbli kwa wiki lakini vimefutiliwa mbali.