Wabakaji Waachiwa Huru, Sababu? Sura ya Aliyebakwa Haivutii!

WANAUME wawili waliachiliwa huru na mahakama ya Italia kwa makosa ya kumbaka mwanamke, baada ya majaji kuamua kuwa mwathirika ana ‘maumbile ya kiume’ na hivyo hangemvutia mbakaji.

 

Wawili hao, ambao wote ni wa miaka 22 waliachiliwa mnamo 2017, lakini sababu ya kuachiliwa kwao ilielezwa Machi, wiki iliyopita, wakati mahakama ya rufaa iliamrisha washtakiwe tena.

 

Majaji walisema kuwa washtakiwa walibaini kuwa mwathiriwa hakuwa na maumbile ya kuvutia, kwani hata mmoja wao aliandika namba yake ya simu kwa jina la  ‘Viking’ kuashiria kuwa maumbile yake hayakuvutia.

 

Mamia ya raia Jumatatu walikusanyika nje ya mahakama hiyo ya Ancona na kuandamana kupinga uamuzi huo wa majaji. Waandamanaji hao zaidi ya 200 waliilaumu mahakama kuwa na upendeleo. Washukiwa walishtakiwa mnamo 2016 kwa kosa la kumbaka mwanamke mnamo 2015, lakini korti ikatupilia mbali mashtaka hayo, ikisema maelezo ya mwathirika hayakuwa ya kuaminika.

 

Mwanamke huyo alikuwa amedai kuwa alibakwa na mwanamume wakati mwenzake alikuwa akitazama.  Ni baada ya watu hao kumwekea dawa katika kinywaji. Madaktari walisema majeraha yake yalionyesha kuwa alibakwa na kuwa damu yake ilipatikana na chembechembe za dawa.

 

Lakini majaji waliamua kuwa  hilo lisingewezekana kwani mwathirika ndiye alipanga mkutano baina yao jioni hiyo kama ilivyoripotiwa.

 

Walisema kuwa “mwanamume anayetuhumiwa kumbaka hata hakumpenda msichana huyo, kwani hata alinakiri nambari yake ya simu kwa jina la utani la  ‘Viking’,  kuashiriahakuwa chochote, si mwanamke, bali kiumbe cha dume. Picha iliyo katika faili yake ilithibitisha hili,” alisema Jaji.

Kesi hiyo itasikilizwa tena na mahakama nyingine ya Perugia katika tarehe itakayoamuliwa.

Toa comment