The House of Favourite Newspapers

Wabongo Waliozamia Sauzi Kinyemela Wahukumiwa Jela – Video

0

MAHAKAM ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kwenda jela miezi sita bila faini washtakiwa 22 raia wa Tanzania baada ya kukutwa na hatia ya kutofuata utaratibu wa kuondoka nchini bila kibali na kuelekea nchini Afrika Kusini kinyume cha sheria.

 

Waliohukumiwa ni Kabila Hussein, Ally Hassan, Jamalino Rashid, Abadi Nassoro,Mzazuri Mohamed, Mohamed Said, Masoro Musa, Mneka Mehra, Waziri Adam, Said Salum, Chuwa Sadiki. Washtakiwa wengine ni Idali Charles, Ibrshim Mohamed, Jafari Zebra, Omare Fizo, Mbuna Edson, Ulembo Azide, Fizo Charles, Salim Kassim, Macalot Alex, Kayeng Winston na Mnangwa Rajabu.

 

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo amesema kwa kuwa washtakiwa hao wamekiri kutenda kosa hilo hivyo mahakama hiyo inawapa adhabu ya kifungo cha miezi sita jela kutokana na kuisababishia hasara serikali ya kuwasafirisha.

 

Mwaikambo amesema kwa kuwa washtakiwa hao wana nguvu ya kufanya kazi hivyo waende wakatumikie na wakafanye kazi wanapokuwa gerezani.

 

“Nyie vijana bado wote mnanguvu na mnaweza kufanya shughuli za kujenga taifa, mmeamua kuiingizia serikali hasara mmesafirishwa na ndege hivyo kutokana na hilo ninawahukumu kwenda jela miezi sita,” amesema Mwaikambo.

 

Awali wakili wa Serikali, Shija Sitta alidai kuwa haoni sababu ya Washtakiwa hao kutoka nchini na kwenda Afrika ya Kusini badala yake wameidhalilisha nchi ya Tanzania na akaiomba mahakama iwape adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

 

Katika kesi yamsingi inadaiwa Januari 21, 2020 katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam tarehe isiyojuliksna na mipaka isiyojulikana washtakiwa hao walitoka nchini na kuelekea nchini Afrika Kusini kinyume na sheria.

 

Leave A Reply