Wabunge Chadema Watinga Bungeni

Baadhi ya wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameendelea kuhudhuria vikao vya bunge kinyume na agizo la Mwenyekiti wao,  Freeman Mbowe, la kuwataka kutoingia Bungeni kutokana na ugonjwa wa Corona  (COVID-19)

Miongoni mwa wabunge ambao walionekana kuingia ni Mbunge wa Momba David Silinde , Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare, Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara Joyce Sokombi, Mbunge Viti Maalum Babati Manyara, Anna Gidalia, Rose Kamili, Jafali Michael, Mbunge wa Viti Maalumu, Lucia Mlowe, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha Mhe. Cecilia  Paresso, Mbunge wa moshi vijijini, Anthony Komu, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza, Susan Masele, na Mbunge wa jimbo la Karatu Mhe. William Qambaru.


Toa comment