The House of Favourite Newspapers

WABUNGE WA CCM WAMUAGA KINANA

Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Abdurahmani Kinana (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally.
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wabunge katika hafla aliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya wabungea wa CCM akizungumza katika hafla ya kumuaga Katibu Mkuu Mstafu Abdulrahman Kinana na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wabunge katika hafla aliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma jana.
Sehemu ya wabunge wakifuatilia Hafla hiyo
Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally akizungumza na wabunge katika hafla ya kumuaga Katibu Mkuu Mstafu Abdulrahman Kinana iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Kassim Majaliwa amemkaribisha Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally na kumuaga mtangulizi wake Abdulrahman Kinana.

 

Majaliwa ambaye pia ni Waziri Mkuu amesema ushirikiano uliopo baina ya wabunge wa chama hicho ni nguzo ya ushindi katika uchaguzi.

Amemhakikishia uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani wataibuka kidedea.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo Juni 19, 2018 katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM jijini Dodoma.

Majaliwa amesema ushirikiano uliopo baina ya wabunge umefanikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 chini ya Kinana, huku akimuahidi Dk Bashiru kuendeleza ushirikiano huo.

“Ili tushinde jitihada za mbunge ni kubwa na hatuko tayari kupoteza kiti chochote katika maeneno yoyote yale,” amesema Majaliwa.

Amesema, “Tutakulinda, tutakusemea na wabunge wako tayari kukupigania. Tutashinda uchaguzi wa serikali za mitaa. Tukuhakikishie uko katika mikono salama.”

Majaliwa amesema wanamshukuru Kinana kwa kuwa wamefanya naye kazi kwa weledi, jitihada na kwa mafanikio makubwa.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya wabunge wa CCM, Margaret Sitta amesema kama wangeulizwa bungeni, wanaosema Kinana astafuu hajui ambaye angesema ndiyo ila wengi wangesema siyo, huku akiungwa mkono na wabunge waliosema “siyooooooo”

“Ulitupenda, ulitutetea na ulikuja kwetu na kutusikiliza. Kinana ulikipenda chama na kama mtakumbuka alipokuwa katibu mkuu alikitumikia chama kwa moyo wote na alipopata ukatibu mkuu alizunguka nchi nzima, alichangamsha chama ndiyo ukweli wenyewe,” amesema Sitta.

Amesema, “Ulikuwa mkweli, ulisaidia kukosoa, ulitusifia na kuhimiza sana kutumikia wananchi… asante sana baba ulichangamsha na ulihiimiza tuimarishe chama na kuwa wamoja na kushikamana.”

Comments are closed.