Wabunge wa upinzani watoka tena bungeni leo
Hata hivyo, licha ya baadhi ya wabunge wa Ukawa akiwemo Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea kuendelea kuomba mwongozo, naibu spika aliwanyima nafasi hiyo, jambo lililosababisha wasusie kikao hicho na kutoka nje huku wakilalamika kwamba wamezibwa midomo.