The House of Favourite Newspapers

Wachezaji Simba, Benchi la Ufundi Watua Bungeni

0

KIKOSI cha Klabu ya  Simba leo Februari 3, 2021, baada ya kutinga makao makuu ya nchi, Dodoma, kimepata fursa ya kuingia ndani ya Bunge la Tanzania wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez, na Msemaji wa Klabu, Haji Manara.

Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez (kushoto) akiongea jambo na Msemaji wa Klabu, Haji Manara.  wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge la Tanzania.

Miongoni mwa wachezaji walitinga bungeni ni pamoja na Gadiel Michael, Ibrahim Ajibu, Said Ndemla, Shomari Kapombe, Clatous Chama, na Mohamed Hussein.

Wengine ni Kenedy Juma, Hassan Dilunga, Ibrahim Ame, Beno Kakolanya, Aishi Manula, Pascal Wawa, Mzamiru Yassini, na Luis Miquissone.

Benchi la ufundi lilikuwa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, na  kocha msaidizi, Seleman Matola.

Wengine ni Mratibu wa Klabu,  Abbas Seleman, na Ofisa Habari wa Simba Haji Manara.

Wabunge, Mtendaji Mkuu wa Simba, wachezaji na benchi la ufundi wakiwa nje ya Bunge la Tanzania.
Leave A Reply