The House of Favourite Newspapers

Wachimba migodi zaidi ya 400 Afrika Kusini wazuiliwa chini ya ardhi

0

Waasi wachimba madini wamewazuia wafanyakazi zaidi ya 400 chini ya ardhi siku ya Ijumaa katika mgodi wa dhahabu nchini Afrika Kusini, wakati wafanyakazi 250 wameitisha mgomo wao katika mgodi wa platinum, kampuni na wawakilishi wa umoja wa wafanyakazi umesema.

Wachimba dhahabu 447 wamekuwa wakishikiliwa chini ya ardhi mashariki mwa Johannesburg, katika tukio la kujirudia la siku tatu mwezi Oktoba, mwendeshaji alisema.

Tukio la hivi karibuni linafuatia mauaji yaliyotokea wiki hii ya mpelelezi wa kampuni ambaye alikuwa akifuatilia mgomo wa awali, alisema Ziyaad Hassam, mkuu wa sheria katika mgodi wa Gold One ulioko Springs.

Kundi dogo la wafanyakazi waliokuwa wamevaa mavazi ya kujifunika uso walikuwa wakihusika na “suala la mateka” ambalo lilianza wakati wa zamu ya Alhamisi usiku.

Waasi walidhibiti kadi za usalama za kuingia kwenye mgodi “kwa hiyo walishindwa kutoka nje ya machimbo” Hassam aliliambia Shirika la habari.

Wachimba migodi wawili walioweza kutoroka Ijumaa asubuhi walithibitisha matukio hayo kwa utawala.

Zaidi ya wachimba migodi 500 walikwama chini ya ardhi kwa takribani siku tatu katika mwezi wa Oktoba wakati malumbano kati ya vyama vya wafanyakazi vinavyopingana.

Leave A Reply