The House of Favourite Newspapers

Geita: Wachimbaji Wanne Wafariki Dunia Mgodini Baada ya Kufukiwa na Kifusi

0

GEITA: Wachimbaji wadogo wanne wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo madogo ya Nyamalimbe yaliyopo wilayani Geita mkoani hapa.

Watu saba walifukiwa ambapo kati yao watatu wameokolewa na wamelazwa katika Kituo cha Afya Katoro.

Tukio hilo limetokea  saa mbili asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Leave A Reply