The House of Favourite Newspapers

Wadada Wapewa Somo la Kupata Mpenzi wa Kuwaoa

0

ZAMA hizi ni kusaidia kwa kila kitu. Kama wewe ni binti ambaye unatamani na unataka ukute au upate mwanaume wa kukuoa akiwa na kila kitu bila wewe kuvuja jasho au kushiriki, utasubiri sana.

 

Utaendelea kula­lamika kuwa hakuna waoaji bila kujua waoaji wapo lakini nao wana vigezo vyao.

Waoaji wapo ila wewe una ubaguzi, una matabaka, una­taka usihangaishe akili yako kufikiria kuhusu mafanikio bali unataka mafanikio yaliyo tayari. Ni tatizo!

 

Kama una tabia na fikra za aina hiyo wewe ni mwanamke ambaye ni tege­mezi, hata kama ukipewa mtaji wa milioni bado unaweza kuumaliza kwa fikra kuwa wakukupa mtaji mwingine yupo.

 

Kama wewe unach­agua mwanaume mwenye kazi, nyumba nzuri, gari na msha­hara hata wanaume nao wanahitaji na wanachagua mwan­amke mwenye kujita­mbua, mwanamke mwenye kujisima­mia.

 

Wanataka mwa­namke mwenye kazi, mwanamke ambaye anaweza akasimama yeye mwenyewe hata kama mwanaume atakuwa kwenye matatizo ya kiuchumi au kiafya.

Kwa sasa hakuna mwanaume ambaye anapenda kuoa au kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye yupoyupo, hana kazi.

 

Hilo ni sumu kwa sasa kwa sababu akikuoa au aki­anzasha uhu­siano na wewe itakuwa shida sana kwani kila kitu utakuwa un­amtegemea yeye.

Kama ni binti na hujaolewa au hujatamkiwa habari za kuolewa basi jiulize sana inawezekana mwenendo na tabia yako ya kuchagua wachumba na kutaka mambo makubwa ndiyo hasa ki­ nakufelisha.

 

Mwingine unaweza kukuta ukichagua mwanaume wa kuku­oa kwa mbwembwe nyingi kwa sababu unajiona bado binti, bado unalipa lakini kama hujui ndugu yangu muda unaenda na mambo yanazidi kubadilika kila kukicha.

Simaanishi usichague la hasha ila jaribu kuangalia maisha nje ya muonekano wa mtu kwa sababu unaweza kucha­gua mwanaume mwenye kazi, nyumba na gari zuri lakini mwisho wa siku akawa hana mapenzi ya kweli.

 

Nini kitakacho­fuatia kama siyo penzi lako kuwa la mateso?

Kwa binti ambaye anahi­taji kuolewa si vyema sana akaangalia pesa, mali au elimu ya unayetaka akuoe bali angalia utu na namna ambavyo mwa­naume anakujali.

Ana upendo? Ana uw­ezo mzuri wa kufikiri ka­tika maisha ya baadaye? Unaposhiriki kwenye mafanikio ya mumeo inakuwa ni jambo zuri na la kujivunia kuliko kukuta kila kitu kikiwa kwa mwanaume, hii itakufanya uwe kama unanyanyasika.

 

Hata ikitokea mmek­waruzana kidogo basi anakutimua na matusi juu kuwa huna chako pale.

Na ukiangalia katika uhalisia huna chako zaidi ya wewe na ma­begi yako ya nguo.

Usijione kama ni mwanamke mwenye ba­hati, furaha na raha sana ka kumpata mwanaume ambaye umemkuta na kila kitu, sikia uchungu na mwambie au mfanye jambo fulani ambao na wewe utashiriki kwa asilimia zote. Kidogo itakusaidia.

Kwa ushauri zaidi like Facebook Page yetu ya Mimi na Uhusiano, Insta@mimi_na_uhusiano au jiunge na Mi&u WhatsApp kwa kutumia namba ya juu.

 

Leave A Reply