The House of Favourite Newspapers

Wadau Wafanya Mkutano Kudhibiti Ukatili wa Kimtandaoni Dhidi ya Watoto

Dar es Salaam, 19 Machi 2025: Shirika lisilo la kiserikali la PDF (Peoples Development Forum) kwa kushirikina na wadau kutoka taasisi na mikoa mbalimbali hapa nchini wanaendelea na mkutano wa siku mbili ulioanza jana (Jumanne) Jijini Dar es Salaam, kujadili namna ya kudhibiti ukatili wanaofanyiwa watoto mitandaoni.

Miongoni mwa wadau hao ni maofisa wa Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi, Walimu, Wasaidizi wa Kisheria, Wahadhiri kutoka vyuo vikuu na wengineo.

Katika mkutano huo wadau hao wanajadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo watoto hao na jinsi ya kukabiliana nazo.

Akizungumza na wanahabari kwenye ufunguzi wa mkutano huo Mkurugenzi wa PDF Tanzania, Ramadhan Masele amesema lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha wadau hao ili kujadili jinsi ya kufanya ili kuwakomboa watoto ambao kwa sasa ndiyo waathirika wakubwa wa kutumiwa vibaya mitandaoni. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN/ GPL